Breaking News

WADAU WASHAURIWA KUTOA ELIMU YA MALEZI KWA WASAIDIZI WA KAZI ZA NDANI KUONDOKANA NA VITENDO VYA UKATILI KWA WATOTO

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Mtoto kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi.Mwajuma Mwagwiza (kushoto) akizungumza na wakati akifungua kikao kilichokutanisha wadau wa utekelezaji wa Mpango Mkakati wa kitaifa wa kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto katika kipengele cha nne kinachohusu malezi na makuzi kwa mtoto jijini Dodoma kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Mtoto kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi.Grace Mwangwa.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Mtoto kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi.Grace Mwangwa (kushoto) akitoa ufafanuzi kuhusu Mpango Mkakati wa kitaifa wa kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto katika kikao kilichokutanisha wadau wa utekelezaji wa Mpango Mkakati wa kitaifa wa kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto katika kipengele cha nne kinachohusu malezi na makuzi kwa mtoto jijini Dodoma.
Mwakilishi wa Shirika la IRCPT Bw. Rogers Fungo (kulia) akichangia katika kikao kilichowakutanisha katika kikao kilichokutanisha wadau wa utekelezaji wa Mpango Mkakati wa kitaifa wa kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto katika kipengele cha nne kinachohusu malezi na makuzi kwa mtoto jijini Dodoma.
Mwakilishi wa Shirika la C-SEMA Bw. Michael Marwa (kulia) akichangia katika kikao kilichowakutanisha katika kikao kilichokutanisha wadau wa utekelezaji wa Mpango Mkakati wa kitaifa wa kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto katika kipengele cha nne kinachohusu malezi na makuzi kwa mtoto jijini Dodoma.
Mwakilishi wa Shirika la Plan International Bi. Oliver Kapaja (kushoto) akichangia katika kikao kilichowakutanisha katika kikao kilichokutanisha wadau wa utekelezaji wa Mpango Mkakati wa kitaifa wa kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto katika kipengele cha nne kinachohusu malezi na makuzi kwa mtoto jijini Dodoma.
Mwakilishi wa Shirika la WAY-Batwana Bi. Grace Muro (kushoto) akichangia katika kikao kilichowakutanisha katika kikao kilichokutanisha wadau wa utekelezaji wa Mpango Mkakati wa kitaifa wa kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto katika kipengele cha nne kinachohusu malezi na makuzi kwa mtoto Dodoma.
Baadhi ya wadau wakifuatilia hoja mablimbali zilizokuwa zikitolewa katika kikao kilichokutanisha wadau wa utekelezaji wa Mpango Mkakati wa kitaifa wa kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto katika kipengele cha nne kinachohusu malezi na makuzi kwa mtoto jijini Dodoma.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
………………………………………………………………………

Na Mwandishi Wetu Dodoma

Wadau wa masuala ya Malezi na Makuzi kwa mtoto wameshauriwa kujikita katika kutoa elimu hiyo kwa wasaidizi wa kike na wa kiume wa kazi za ndani ambao wengi wao wanatumika na watanzania walio wengi katika kulea watoto wao ili kuondokana na vitendo vya ukatili kwa watoto hao.

Hayo yamebainika katika kikao kazi kilichofanyika leo jijini Dodoma kilichowakutanisha wadau wa utekelezaji wa Mpango Mkakati wa kitaifa wa kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto katika kipengele cha nne kinachohusu malezi na makuzi kwa mtoto.

Akizungumza suala hilo katika kikao hicho Afisa Ustawi wa Jamii Mwandamizi Bi. Amina Mafita amesema kuwa Wadau wanafanya kazi kubwa ya kutoa elimu kwa wazazi, walezi na watoto kuhusu malezi na makuzi kwa watoto wao lakini kwa kiasi kikubwa kundi la wasaidizi wa kazi za ndani wameachwa nyuma wakati kwa asilimia kubwa wao ndio wanatekeleza majukumu ya malezi kwa watoto.

Ameongeza kuwa vitendo vingi vya ukatili vinavyofanywa kwa watoto hasa watoto ambao bado hawajaweza kujieleza vimekuwa vikifanywa na wasaidizi hao huku msukumo mkubwa wa wadau ukiwa umewekwa kwa wazazi na walezi kupata elimu ya malezi na makuzi wakati kwa muda mwingi watoto wamekuwa wakikaa na wasaidizi hao.

Akifungua kikao hicho Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Mtoto kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Mwajuma Magwiza amesema kuwa Wizara imewakutanisha wadau hao ikiwa ni muendelezo wa vikao vya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) ambao utatekelezwa kwa ushirikiano na wadau katika seshemu ya nne ya utekelezaji wa Mpango huo wa Malezi na Makuzi kwa Mtoto.

Ameongeza kuwa utekelezaji wa Mkakati huo kwa eneo la nne la utekelezaji la Malezi na Makuzi kwa mtoto utakuwa msaada wa kutekeleza mpango huo ili kuwezesha kuondokana na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2022 kwani eneo hilo limekuwa likisababisha sana vitendo vya ukatili kwa watoto ambapo kwa asilimia kubwa wazazi na walezi wameshindwa kutimiza wajibu wao.

Naye Mwakilishi wa Shirika la Way-Batwana Bi. Grace Muro amesema Shirika lake limejipanga kuondokana na vitendo hivyo kwa kuwa na Mpango kwa utoaji wa elimu ya Malezi na Mkuzi kwa wanafunzi wa Shule za Sekondari ambapo utasaidia kuongeza nguvu zaidi za kutekeleza Mpango wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA).

No comments