Breaking News

FAHAMU FAIDA YA KUTUMIA MBOGA YA KABICHI KWA CHAKULA NA TIBA

Kabichi linaweza kuliwa bichi, Likichanganywa kwenye kachumbari au kupikwa na kula. Kabichi lina kalonzi kidogo Lakini lina vitamini c nyingi sana. Wataalam wanatuambia kabichi lina madini ya calcium na chuma pia yapo.

Linaponyesha vidonda vya tumbo linapotumika katika mfumo wa juisi.ukishamaliza kutengeneza juisi ni vyema kuinywa mara moja kabla haijakaa sana.

Glasi moja ya juisi ya kabichi inasaidia kuondoa mhemko au msongo kwenye Akili, huondoa woga,
kuumwa kichwa n.k husaidia sana kuponya kichwa hasa kichwa kinachouma mchana.

Ukijisikia vibaya kunywa juisi ya kabichi si vibaya kama Utachanganya na Asali au juisi ya karoti
kwani nayo ina faida nyingi kwa Afya ya mwanadam.

Kwa tatizo la pumu:

Chukua ml 200 za juisi ya karoti ongeza ml 100 za juisi ya spinachi kunywa mara 3 kwa siku kwa
muda wa miezi mitatu utapona kabisa. katika hiyo miezi mitatu kula kachumbari ya kabichi na
spinachi bila chakula kingine muda wowote.

Unakula kachumbari peke yake bila kuchanganya na mlo mwingine. changanya nyanya, kitunguu
maji na limao kidogo.

Kuondoa maji meupe katika macho changanya juisi ya kabichi na juisi ya kitunguu na Asali kisha tia
machoni matone yanasafishika na kuondoka kabisa yale maji meupe.

Ugonjwa wa saratani (cancer) ni miongoni mwa magonjwa hatari yanayosumbua watu
duniani hivi sasa, Tanzania ikiwemo.

Wagonjwa wanaongezeka kila kukicha katika Hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam, ambayo ni maalum kwa ugonjwa huu.

Katika makala ya leo, tutajifunza faida za kabichi katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo, licha ya kuchukuliwa kama ni mboga ya kimaskini na ambayo huliwa kwa shida zaidi kuliko kimanufaa ya kiafya.

Ingawa inaonekana kuwa kabichi ni miongoni mwa mboga za majani zinazolimwa kwa wingi
na kusambazwa kwenye masoko mengi nchini, hasa katika miji mikubwa, lakini ni watu wachache sana wanaopenda kula mboga hii.

Katika miji mikubwa, kabichi inatumika zadi kwa walaji wa chips. Hata hivyo hawaitumii
ipasavyo kwa sababu huwa inapikwa na kukaangwa kwa mafuta kwa muda mrefu na hivyo kupoteza baadhi ya virutubisho vyake muhimu.

KINGA DHIDI YA SARATANI
Miongoni mwa faida nyingi zinazopatikana kwa kula kabichi (nyeupe na nyekundu), inayoongoza ni ile ya kutoa kinga dhidi ya ugonjwa hatari wa saratani.

Inaelezwa kuwa zaidi ya tafiti 475 zimefanyika kuhusu virutubisho vinavyopatikana kwenye kabichi na kuthibitisha kuwa vina uwezo wa kuzuia ugonjwa wa saratani na wakati mwingine kutibu.

Kabichi imeonekana kuwa na uwezo wa kipekee katika kupambana na ugonjwa huu kutokana na kuwa na kiasi kikubwa cha aina tatu muhimu za virutubisho;

‘Antioxidant’, ‘Anti-inflammatory’ na ‘Glucosinolates,’ ambazo zina uwezo wa kudhibiti magonjwa nyemelezi kadhaa ambayo husababisha saratani za aina mbalimbali mwilini.

Kwa kuzingatia madhara na mateso yatokanayo na ugonjwa wa saratani, na kwa kuzingatiaupatikanaji wa kabichi usiokuwa na gharama, huna sababu ya kupuuzia ulaji wake. Laiti kama watu wote tungejua sawasawa faida za kabichi, bila shaka mboga hii ingekuwa ghali kuliko hata samaki.

AHUENI YA VIDONDA VYA TUMBO
Mbali ya kuwa na uwezo wa kutoa kinga dhidi ya ugonjwa wa saratani, juisi ya kabichi inaelezwa kuwa na faida nyingi tumboni, hasa kwa wale wenye matatizo ya vidonda vya tumbo (peptic ulcers). Ikitumika mara kwa mara huwa kama tiba kwao. Hali kadhalika mfumo wa usagaji chakula tumboni, huwa imara.

HUIMARISHA MFUMO WA MOYO
Utafiti mwingine uliofanyika kuhusu kabichi umeonesha kuwa mboga hii huimarisha mfumo mzima wa moyo kwa kudhibiti utengenezwaji wa lehemu (cholesterol) mbaya mwilini ambayo inapozidi mwilini, husababisha matatizo ya moyo.

VITAMINI ZINAZOPATIKANA KWENYE KABICHI
Ndani ya kabichi, kuna kiwango cha kutosha cha aina mbalimbali za vitamin, hususan Vitamin K, Vitamin B1, Vitamin B2, Vitamin A na Vitamin C. Aidha, kabichi ina kiasi kingi cha kambalishe (fiber) Manganizi (Manganese), Potashiamu (Potassium) na Fatty-3 acids. Vyote hivi ni kinga ya
mwili dhidi ya magonjwa nyemelezi.

Ili kupata faida za kabichi na kujenga kinga imara dhidi ya magonjwa ya saratani, weka mazoea ya kula kabichi mara kwa mara, angalau mara tatu kwa wiki, kwa namna ambayo utaona mwenyewe inafaa, iwe kama mboga au kachumbari.

No comments