Breaking News

OPERESHENI BENDERA YATUA WILAYANI KINONDONI, "HAMASA NDIO UHAI WA JUMUIYA"-BOMBOKO


Ziara ya Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Taifa kukagua Vikundi vya Hamasa Mkoa wa Dar es Salaam Wilaya ya Kinondoni.

Katibu Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM TAIFA ndugu Hassan Bomboko Leo ameendelea na ziara ya kimkakati ya Oparasheni Bendera inayolenga Kurejesha Uhai wa Jumuiya kwa kutumia HAMASA Kuanzia Ngazi ya Tawi, Kata, Wilaya na Mkoa

Katika ziara hiyo iliyofanyika wilaya ya kinondoni ndugu Hassan Bomboko alitembelea kata ya Tandale kata Kusimika Bendera katika Nyumba za Mabalozi wa CCM

"Ndugu zangu wana kinondoni leo tumefika hapa na mpango wetu huu wa kuitumia Hamasa kama Njia ya Kurejesha Uhai katika Jumuiya yetu, Dhamira ya Oparasheni hii ni kuhakikisha tunavitambua vikundi vya hamasa, tunavipa nguvu, kuvijengea uwezo na kuvirasimisha katika utaratibu unaoeleweka, Lakini leo tupo hapa ikiwa ni sehemu ya kuwatia moyo mabalozi wetu kwa kutambua na kuthamini mchango wao katika kukitumikia na kukiletea ushindi Chama Cha Mapindizi Katika Chaguzi zote

Rai yetu kwa viongozi wetu hawa mabalozi waendelee na wito huu wa kukipigania Chama na kukiletea ushindi katika Uchaguzi Ujao wa serikali za mitaa na Vitongo/ Vijiji" Alisema katibu Hamasa akikabidhi na kusimika bendera katika Nyumba za mabalozi

Pamoja na Mambo mengine Mkuu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi alihitimisha kwa kwa kukagua vikundi vyote vya hamasa wilaya ya Kinondoni na Kisha kuwapa uwelewa mpana wa Kiitikadi, Kisera na Kuwataka wahamasishaji wa ngazi ya kata na matawi kufanya Jitihada ya Kuifahamu vyema Misingi, Imaani na Falsafa ya Chama Cha Mapinduzi ili wapeleke Uwelewa huo kwa kwa wananchi

Kupitia sanaa na Hamasa kwa Ujumla tunao wajibu wa kuhamasisha vijana wenzetu Kufanya kazi kwa Juhudi katika ujenzi wa Taifa letu

Mwisho nifikishe Salaamu za Mwenyekiti wa Vijana Taifa Comrade Kheri Denice James ameendelea kunisistiza niwaeleze Vijana wa Mkoa huu wa Daresalaam kujiandaa na Uchaguzi Ujao, kama vijana tunao wajibu wa kuhakikisha CCM inashinda kwa kishindo na kushika hatamu katika Maeneo yote, Mwenyekiti ameniagiza niwaambie tuendelee kuunga mkoni utekelezaji wa ilani yetu ya CCM 2015 - 2020." Aliyasema haya katibu wa idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM TAIFA akiwahutubia wana kinondoni

Imetolewa na
Idara ya Uhamasishaji na Chipukiz UVCCM TAIFA

MATUKIO KATIKA PICHA
Katibu Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Taifa Ndg Hassan Bomboko akiwasili Wilayani Kinondoni, akiwa ameambatana na Viongozi mbalimbali wa UVCCM.




No comments