Breaking News

KUELEKEA KILELE CHA MAADHIMISHO YA MIAKA 42 YA CCM , BI. NICE MUNISSY AAMSHA ARI YA MABINTI KUJITAMBUA.

Mjumbe Baraza Kuu UVCCM Taifa (Kilimanjaro) Ndg Nice Munissy akizungumza na Mabinti wenzake kwenye Uzinduzi wa Binti CCM Kampeni
Mjumbe wa Baraza kuu la UVCCM Taifa NICE MUNISSY katika mazungumzo na BINTI CCM KAMPENI amesema, huwezi kuzungumzia UHURU WA SERIKALI YA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA bila kumtaja/kumzungumzia Binti wa CCM ambapo ametoa mifano ya mabinti waliopambana kuhakikisha wanatoa mchango mkubwa enzi zao kuhakikisha uhuru wa Tanzania, ameeleza kuwa Leo tuna Amani tuna Uhuru wa kuongea tunapata haki zetu za msingi kwa kiasi kikubwa kwa sababu ya UHURU tulionao lakini sio tu Uhuru ni kwasababu tuna Chama Imara kinachoweza kuisimamia serikali chama ambacho Msingi wake ni utu,Chama kinachoamini katika Haki na Usawa, Na Hivyo BINTI CCM KAMPENI inalenga kuuhisha uimara wa binti halisi wa CCM Binti anaeweza kuaminiwa na kufanya maamuzi kwa mustakabali wa Taifa letu,

Bi.NICE MUNISSY Ame wasaa mabinti kutizama aina ya watu wanaowazunguka na kuepuka kuwa na idadi kubwa ya watu hususani marafiki wasio natija “Tambua aina ya watu waliokuzunguka, Punguza idadi ya marafiki wasio na tija kwako,Epuka watu wanaokurudisha nyuma katika safari yako ya mafanikio” NICE MUNISSY MJUMBE WA BARAZA KUU TAIFA ANAEWAKILISHA VIJANA WA MKOA WA KILIMANJARO

Vilevile ameongeza kwamba ni muhimu kujua aina ya watu walioyuzunguka watu tunaotaka kuwaongoza,Changamoto zinazowakabili na kuwa na mkakati thabiti utakaotumika kutatua changamoto hizo ikibidi kuzibadili kuwa Fursa.

No comments