Breaking News

KATIBU TAWALA MARA AVUTIWA NA KASI YA UJENZI WA KITUO CHA AFYA MAGENA.

"Tukutane Kazini" RAS Caroline Mthapula akiwasili Kituo cha Afya Magena tayari kwa kukikagua
RAS Caroline Mthapula akiendelea na ukaguaji wa ujenzi wa Kituo cha Afya Magena Wilayani Tarime
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Mhe. Caroline Mthapula akishiriki ujenzi wa kituo cha Afya Wilayani Tarime

Na Mossy Magere
Katibu Tawala mkoa wa Mara,Caroline Mthapula ameridhishwa na kasi ya utekelezaji wa ujenzi wa kituo cha afya Magena wilayani Tarime. 

Akiwa kwenye ukaguzi wa miradi wilayani Tarime Caroline alipata fulsa ya kutembelea kituo hicho cha kisasa kinachojengwa na Halmashauri ya Tarime Mji.
"Naona mnaendelea vizuri,kasi ya mafundi iko vizuri nawatakia kazi njema"alisema Caroline

Katika ziara hiyo katibu tawala Mkoa aliongozana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Tarime mji Elias Nturuhungwa pamoja na wataalam wa mkoani na wa Halmashauri hiyo.

No comments