Breaking News

USHAIRI: "KIDONDA CHA HUBA"

Ushairi: KIDONDA
Mshairi: HAMISI A.S KISSAMVU
0715311590
kissamvujr@gmail.com
kutoka (Baitu shi'ri)
MABIBO DSM

1. Kidonda hiki kidonda, cha mahaba ni msiba. 
Kilio kitakutanda, mwilini kikikukaba
Hauchelewi kukonda
Kukonda kutakuwanda,na tibaye huwa haba
Siku zitazidi kwenda.chakutafuna ja buba
Sio kale hata sasa huponi donda la huba

2. Kinadanganya kupona,juu kuweka kigaga
Kumbe uzima hapana, na mwili chauvuruga
Muumwa talia sana
Sana peke akibana,fikira za mvuruga
Akikumbuka ya jana, kwa siha aliwakoga
Sio kale hata sasa huponi donda la huba

3. Wengi kinawadhuru, wala hakuna jabari
Kikikupata shukuru, muombe dua kadari
Kidonda hiki hatari
Hatari chafunga nuru, huwi mwenye kufikiri
Zinakupotea heri, kila ulacho shubiri
Sio kale hata sasa huponi donda la huba

4. Aondoke mahabuba, alokukaa moyoni
Alokujaza kwa huba, ukapoteza uoni
Ni mauko ya mahaba
Mahaba tena ni haba, yatakuwa henzerani
Utabaki na ukuba, mziba pengo ninani?
Sio kale hata sasa huponi donda la huba

5. Wala hakuna tabibu, wa bara hata mrima
Awezaye kulitibu, ukarejea uzima
Hata walio janibu
Janibu nako ni tabu, hili donda la zizima
Vijana na mashaibu, kilindini wamezama
Sio kale hata sasa huponi donda la huba

6. Hapa tamati ya mbeko, nayasitisha maneno
Yakata huku na huko, mkato wa msumeno
Donda halina kifano
Kifano chake kihako, haya sifanye bishano
Mvuzi wa maandiko, hawezi fanya kiguno
Sio kale hata sasa huponi donda la huba

No comments