Breaking News

UMEME WA GRID YA TAIFA WAWASHWA RASMI WILAYANI LUDEWA, WAZIRI DKT KALEMANI AWAONYA TANESCO


Na Maiko Luoga, Ludewa- Njombe

Hatimae Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe Imeanza Kutumia Umeme wa Grid ya Taifa na Kuachana na Umeme wa Mtambo wa Mafuta Mazito uliokuwa ukitumika Awali wilayani Humo Mtambo ambao unatajwa Kutumia Gharama Kubwa Tofauti na Gharama ya Grid ya Taifa.

Akizungumza na Wananchi wa Ludewa Mjini waliojitokeza katika Mkutano wa Kuzima Mtambo mkubwa wa Mafuta na Kuwasha Grid ya Taifa Waziri wa Nishati Dkt,Medad Kalemani Alisema kuwa Wilaya ya Ludewa Imepata Umeme wa Grid ya Taifa Kupitia Mradi wa Makambako, Songea Kisha Madaba hadi Ludewa Jumla ya Klomita 140.

Aidha Waziri Kalemani Alisema Kuwa Mtambo wa Mafuta Mazito Uliokuwa Ukitumika Awali Ludewa Ulikuwa na Uwezo Mdogo wa Kufua Umeme Wa Megawati 0.5 Ambapo kwasasa Kupitia Grid ya Taifa Serikali Imeamua Kufunga mashine Kubwa yenye Uwezo wa Kufua Umeme Megawati 2 Wakati Mahitaji ya Umeme kwa wakazi wa Ludewa kwasasa Ni Megawati 1.5 Hivyo Kufungwa Mashine ya Megawati 2 Kutasaidia Ludewa kuwa na Umeme wa Ziada.

Katika Hatua Nyingine Waziri wa Nishati Dkt.Kalemani Ametoa Rai kwa Watumishi wa Tanesco Wilaya ya Ludewa Kuhakikisha Kuwa Umeme huo Uliowashwa Rasmi kupitia Grid ya Taifa Haukatiki Ovyo ili Kuisaidia Jamii Kuendesha Shughuli zao kwa Ufanisi Mkubwa Huku akitoa Muda wa Siku tano Kuanzia Jana November 04 kwa Mkandarasi Anaekamilisha Mradi wa Umeme katika Kitongoji cha Ngalawale Kuhakikisha Kuwa Anawasha Umeme katika Eneo hilo na Mkandarasi ameahidi Kukamilisha Ndani ya Muda huo.

Kwaupande wake Mbunge wa Jimbo la Ludewa Mh,Deo Ngalawa Akizungumza kwa Niaba ya Wananchi wa Ludewa ametoa Ombi maalumu kwa Waziri wa Nishati Kupitia Mradi wa Umeme wa Grid ya Taifa Kuwa Vijiji ambavyo vipo jirani na Vile vilivyopitiwa na Grid ya Taifa navyovipate Umeme Kupitia Grid ya Taifa kwakuwa Vijiji Hivyo Vipo Jirani sana Ikiwemo Vijiji vya Ibumi, Maholong’wa, Kitewele, Kipangala, Ugera, Kilondo, Chanjale, Lumbila pamoja na Kijiji Cha Nkanda Mwambao mwa ziwa nyasa. 

Kwamujibu wa Msimamizi wa Mradi huo wa Makambako Songea Alisema Kuwa mradi huo Ulianza Rasmi Tangu Mwaka 2015 na Kukamilika Mwezi october Mwaka huu 2018 Kisha Jana November 04 Waziri wa Nishati Amewasha Rasmi Umeme huo wa Gridi ya Taifa Ambapo Hadi Kukamilika Kwake Mradi huo Umetumia Kiasi Cha Bilioni 216 Pesa za Kitanzania Kutoka Serikali Kuu ya Tanzania Kwakushirikiana na Serikali ya Watu wa Sweeden na Watekelezaji ni Shirika la Tanesco. 

Mh, Edward Haule ni Diwani wa Kata ya Ibumi Pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Licha ya Kutoa Shukrani kwa Serikali Kupitia kwa Waziri Kalemani Pia Alimwomba Waziri huyo Kuendelea Kutoa Ushirikiano wa Karibu kwa Mbunge wa Ludewa Mh,Deo Ngalawa ili Kufanikisha Vijiji vyote Vilivyobaki viweze kunufaika na Nishati ya Umeme kwa Muda Muafaka na Baadhi ya wananchi Wakipongeza Jitihada hizo za Serikali wakisema kuwa Ni Hatua kubwa Kuelekea Tanzania ya Viwanda.

No comments