MAKALA YA LEO: RAIS MAGUFULI NA MIAKA MITATU IKULU
Na Emmanuel J. Shilatu
Napenda kuungana na Mamilioni ya Watanzania kote nchini kusheherekea na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli kutimiza miaka mitatu tangu ale kiapo cha kuwa Rais na Serikali ya awamu ya 5 ianze kazi rasmi.
Ni miaka mitatu yenye matunda ya mapambano dhidi ya maadui zetu Watanzania ambao ni Ujinga, maradhi na umaskini.
Ni miaka mitatu yenye Matokeo chanyA+ ya Tanzania ya Viwanda na mageuzi makubwa ya kiutendaji, uwajibikaji, nidhamu na uadilifu nchini. Hakika, Tanzania imekuwa nchi ya mfano Afrika na Dunia kwa ujumla.
Ni miaka mitatu iliyoifanya Tanzania kuwa bora tena kwenye utawala bora, nidhamu ya kulinda rasilimali zetu, nidhamu ya kupambana na rushwa na ufisadi nchini. Hakika Rais Magufuli ameonyesha kujitoa kweli kweli kwa maslahi mapana ya Watanzania na Taifa kwa ujumla.
Ni miaka mitatu ya Rais Magufuli na Serikali kuonyesha kuwajali zaidi Wanyonge, Wanawake, Vijana na Wazee. Hakuna tena uonevu wala matabaka ndani ya jamii yetu.
Ni miaka mitatu iliyojaa heshima kwa katiba ya nchi, utawala wa sheria, uhuru wa kutosha wa kidemokrasia, ulindwaji wa haki, ulinzi na usalama wa Raia.
Ni ngumu kuchambua kimoja kimoja hadi kumaliza mema yaliyofanyika ndani ya miaka mitatu ya Serikali ya awamu ya 5. Ahsante sana Rais Magufuli kwa uongozi uliotukuka kwa Watanzania.
Watanzania tupo bega bega nawe Rais wetu Mpendwa Dkt. John Magufuli kwenye kila hatua kukupa ushirikiano na tutazidi kukuombea kwa Mwenyezi Mungu kila lenye heri.
Heri ya miaka mitatu ya mafanikio ya Matokeo chanyA+.
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Mbariki Rais Magufuli
Shilatu E.J
No comments