Breaking News

KATIBU WA UVCCM WILAYA YA BUNDA ATEMBELEA KAMBI YA UMOJA WA WASANII WILAYA YA BUNDA


Katibu wa UVCCM Wilaya ya Bunda Ndg Steven E. Shija ametembelea Kambi ya Umoja wa Wasanii Wilaya ya Bunda wanaojiandaa Kurekodi Filamu yao Mpya 

Katibu Shija alipokea Changamoto mbalimbali zinazowakabili Wasanii hao na kuahidi kushirikiana nao kuzitatua ili kuleta Ufanisi katika Kazi ya Sanaa ya Maigizo 

"Niwapongeze kwa Juhudi mlizonazo katika Tasnia ya Sanaa kumbukeni Jamii inawategemea sana kuielimisha, hizi Changamoto mnazopitia ni sehemu ya kuwafanya kuwa Imara, hata dhahabu ili ing'ae lazima ipite kwenye Moto, ninaamini tutashirikiana kikamirifu kutatua Changamoto zinazoikabili Kambi ili kuwafanya mfikie malengo yenu nawashukuru kwa kunialika kuwatembelea" Alisema Shija

Viongozi wa Umoja wa Wasanii Wilaya kwa niaba ya Wasanii waliopo Kambini walimshukuru Katibu wa UVCCM Wilaya kwa kuwa mwepesi kuitikia Wito na kukubali kushirikiana nao kutatua Changamoto za Kambi

TUPO KAZINI

Imetolewa na:-
Ndg Magesa Protas
Katibu Uhamasishaji na Chipukizi Wilaya
Bunda, Mara

No comments