Breaking News

NAIBU WAZIRI SIMA AHAMASISHA MAENDELEO MANGA MTIPA, AVISHWA KIMILA ISHARA YA HESHIMA

Mbunge wa Jimbo la Singida ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Mussa Sima leo amefanya Mkutano wa hadhara eneo la Manga Mtipa. 

Katika mkutano huo ambao pia wakazi wa Manga walimpatia Heshima ya Kimila walimzawadia pia Mbuzi mnyama kwa heshima na kuenzi juhudi anazofanya katika kuwaletea Maendeleo. 

Aidha, Mhe Naibu Waziri akielezea namna anavyoshughulikia changamoto mbalimbali ndani ya Kata ya Mtipa kwa kutaja baadhi ya Changamoto ambazo amezipatia ufumbuzi mfano ,Umeme, Elimu Na vifaa vya Zahanati,Ujenzi wa ofisi ya kata na madarasa katika shule mbalimbali za katani,na pia kuahidi kufanyia kazi ndani ya muda mfupi changamoto za Ubovu wa barabara kuunganisha kata pia wananchi wameomba Mnada wa Manga kuwanufaisha pia Wana Manga kwa kurejeshewa asilimia na Mwisho wameomba Kuanza mchakato wa ujenzi wa Shule nyingine ya Sekondari maana iliyopo ni mbali 
Nae mhe Naibu Waziri ameahidi kuzitafutia majawabu Changamoto hizo kwa muda mfupi. 

Singida Mjini Tupo Kazini.

No comments