Breaking News

MWASELELA: SIACHI KUITUMIKIA JAMII YA WATANZANIA

Mdau wa Maendeleo nchini Ndugu Ndele Mwaselela (Kushoto) amesema hatoacha kuitumikia jamii katika maisha yake yote atakayojaliwa na Mungu.

Hayo ameyasema leo Tarehe 05/11/2018 mbele ya waandishi wa habari wa ITV na TBC waliomtembelea ofisini kwake Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupata ufafanuzi wa masuala ya Maendeleo anayofanya katika jamii kwa miaka mitatu ya Rais Dkt John Magufuli.

Mwaselela amewahimizi Watanzania wote kujenga utamaduni wa kuipenda nchi yao na watu wao hasa kuwahurumia wanyonge kwa kuwa waadilifu na wazalendo ili kuijenga Tanzania salama isiyokuwa na ubaguzi wa aina yeyote.

Katika mahojiano hayo, amewasihi Watanzania kujenga na kuendeleza misingi ya kuvumiliana katika ujengaji wa hoja kwenye mijadala, kwasababu binadamu hutofauyiana katika utashi na maono.

"Bnadamu hutofautiana hata kama wana malengo sawa, hivyo ni vema tukaendelea kuhubiri uvumilivu na ustamilivu wakati wote ili amani iendelee kutamalaki katika nchi yetu." Ameeleza Ndele Mwaselela.

No comments