Breaking News

MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA AWAPA MAAGIZO HAYA WAKUU WA MIKOA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu amewaagiza wakuu wa mikoa nchini kuhakikisha kuwa wanasimamia vizuri taarifa za wajawazito na afya za watoto katika kila kata, kuhakikisha taarifa zote zinazohusu afya ya uzazi zinawafikia na wampelekee, ripoti kila baada ya miezi sita. 

Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo leo Novemba 6, jijini Dodoma katika uzinduzi wa kampeni ya kitaifa inayolenga kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi na vifo vya watoto wachanga nchini iliyopatiwa jina la 'Jiongeze! Tuwavushe Salama'. 

Kampeni ambayo madhumuni yake kuhamasisha viongozi wa serikali, viongozi wa dini, mashirika yasiyo ya kiserikali, wadau wa maendeleo, watoa huduma za afya, familia na jamii kwa ujumla ili kuchangia katika juhudi za taifa za kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi na vifo vya watoto wachanga. 

"Naagiza kila Mkuu wa Mkoa, aifanye ajenda ya uzazi iwe ya kudumu katika vikao vya halmshauri kuu za mikoa (RCC) na mfuatilie taarifa zote za wajawazito katika kila kata ziwafikie, naamini halitoshindikana ninachohitaji ni uwajibikaji", amesema Mama Samia.

Makamu wa Rais ameongeza kuwa, "Ifike wakati jamii kwa pamoja iwajibike katika kuungana na kumpatia mwanamke faraja wakati wa kujifungua na tuachane na kauli kwamba mwanamke atazaa kwa uchungu, hebu tuwapunguzie uchungu huo".

Kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Afya mwaka 2017, zinaonyesha kuwa wanawake milioni 2.2 hubeba ujauzito kila mwaka na asilimia 85 hujifungua salama na asilimia 15 pekee ndio hupata matatizo wakati wa ujauzito na wakati wa kujifungua.

No comments