Breaking News

MWENYEKITI UVCCM KASKAZINI PEMBA NDG YAHYA KHAMIS ALI AZUNGUMZA NA WANAFUNZI KIDATO CHA NNE, AWATIA NGUVU

Siku ya Jumamosi ya tarehe 3/11/2018, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kaskazini Pemba Ndg Yahya Khamis Ali alipata nafasi ya kuzungumza na wanafunzi wa Mwitani High School wanaoanza mitihani yao ya Kidato cha Nne leo Jumatatu ya tarehe 5/11/2018. 

Ndg Yahya Khamis Ali amewapa nasaha wanafunzi na kuwaasa kuongeza bidii kipindi hiki cha mitihani na asiwepo wa kukata tamaa ama kuchoka. 

"Jitahidini kufanya mitihani yenu bila ya hofu na msije mkafanya udanganyifu, tambueni serikali imeandaa wasimamizi wazuri wa kusimamia mitihani yenu hivyo mjiamini" alisisitiza Mwenyekiti huyo wa UVCCM Mkoa wa Kaskazini Pemba Ndg Yahya Khamis Ali. 
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kaskazini Pemba Ndg Yahya Khamis Ali akisisitiza jambo mbele ya wanafunzi wa Kidato cha Nne

No comments