Breaking News

KATIBU WA CCM (M) NJOMBE NDG PAZZA MWAMLIMA AUBARIKI UJUMBE KWENDA KUMJULIA HALI MBUNGE WA MAKETE PROF. SIGALLA ALIYELAZWA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI

Na Maiko Luoga, Njombe. 

Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Njombe Wamekutana na Viongozi wa CCM Wilaya ya Makete katika Ofisi ya Katibu wa chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Njombe Ndg. Pazza Mwamlima Kisha wakapokea Taarifa kutoka kwa Viongozi wa CCM wilaya ya Makete Ambao Wanaelekea Dar es laam Kwaajili ya Kumjulia Hali Mbunge wa Makete Mh. Norman Sigala King Aliyelazwa katika Hospital ya Taifa Muhimbili Akiendelea na Matibabu. 

Aidha, Kikao hicho pia Kimehudhuriwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) kutoka Mkoa wa Njombe Ndg. Fidelis Lumato, Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Njombe Ndg Erasto Ngole ambapo kwa pamoja na Katibu wa CCM Mkoa wa Njombe Ndg. Pazza Mwamlima na baadhi ya Wajumbe wengine wamechangia fedha na kuukabidhi ujumbe huo ikiwa ni sehemu ya kufanikisha safari hiyo.

Safari ya Wajumbe watatu Kutoka Wilayani Makete kuelekea Dar es laam Imeongozwa na Katibu wa CCM Wilaya ya Makete Ndg. Lusiano Mbosa aliyewahi Kukitumikia Chama cha Mapinduzi CCM Akiwa Katibu Katika Wilaya ya Ludewa ambapo Safari hiyo ni Maalumu Kwaajili ya Kumjulia Hali Mbunge wa Jimbo la Makete Mhe. Norman Sigalla King. 
Kutoka kushoto: Ndg Erasto Ngole- Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Mkoa wa Njombe, Ndg Pazza Mwamlima- Katibu wa CCM Mkoa wa Njombe na Ndg Fidelis Lumato- Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) wa Mkoa wa Njombe

No comments