MWENYEKITI WA UVCCM TAIFA NDG KHERI JAMES AWA MGENI RASMI KATIKA KUGAWA VIFAA VYA MICHEZO UVCCM MKOA WA IRINGA, ATOA AGIZO KWA MAAFISA MICHEZO
Mwenyekiti wa UVCCM Taifa (MCC) Comrade Kheri D.James ameungana na viongozi wa kata zote 106 za Mkoa wa Iringa katika Ukumbi wa siasa ni kilimo katika ugawaji wa vifaa vya michezo (Jezi na Mipira.
Mwenyekiti wa UVCCM Taifa (MCC) Comrade Kheri D.James Alisisitiza kuhusu Umuhimu wa michezo na kuwataka Kila Wilaya iliyo na Afisa Michezo kuhakikisha wana shirikiana na UVCCM kuandaa na kukuza vipaji pia alimpongeza Mwenyekiti UVCCM Mkoa wa Iringa Comrade Kenani Kihongosi kwa ubunifu, umakini na uchapakazi katika Jumuiya ya Vijana Mkoa wa Iringa alimtaka kuendelea kuwa na Moyo wa kusaidia na kushikamana katika kujenga Chama na Jumuiya katika Mkoa
Komred Kheri D James amewasisitiza vijana kufanya Kazi kwa bidii na kumuunga mkono Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kwa Kazi ya Kipekee anayoifanya kwa watanzania wanyonge, Na Kuwataka vijana kuwapuuza wanasiasa Wanaochonganisha Serikali na wananchi kwa maslahi yao binafsi, Amesema Tanzania ni Nchi Huru Na Haiingiliwi na Mataifa ya Nje katika masuala yake ya Ndani hivyo lazima tumuombee Rais wetu kwa dhamira Njema aliyonayo kwa wananchi wa Tanzania.
Katika mkutano huo Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndg Salim F. Abri aliwapongeza UVCCM Mkoa wa Iringa kwa kazi kubwa wanayofanya ya ujenzi ya kuimarisha Jumuiya na Chama na pia Alionya Makada wanaotafuta Ubunge kufuata Sheria Taratibu na Kanuni za Chama Cha Mapinduzi, atakae kiuka atawajibishwa kwa mujibu wa Vikao Vya Chama, na alisisitiza hatomvumilia mtu yeyote atakichafua Chama Cha Mapinduzi kwa maslahi yake binafsi. Aliwasisitiza Vijana kutotumiwa na watu wenye nia Ovu kwa Chama Cha Mapinduzi.
Akifungua mkutano huo M/Kiti wa UVCCM Mkoa wa Iringa Ndg.Kenani Kihongosi alimshukuru Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndg.Salm F. Abri kwa kuwezesha kutoa vifaa vyote vya Michezo katika kata 106 za Mkoa wa Iringa, na ameahidi kuvisimamia na kuhakikisha vinawafikia walengwa, pia aliwashukuru Vijana wote wa Mkoa wa Iringa kwa ushirikiano wanaoipa Jumuiya ya Vijana Mkoa wa Iringa na akasema watafuatilia kila kata katika Ziara ya kamati ya utekelezaji Mkoa wa Iringa itakayoanza kama vifaa vimewafikia walengwa na akasisitiza viongozi watambue vifaa hivi ni mali ya Jumuiya katika kila kata na sio Mali ya mtu binafsi. Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Iringa alimshukuru tena MNEC Ndg Salim F. Abri kwa kusaidia jumuiya vifaa vya michezo kwaajili ya Vijana wa Iringa.
Katika Tukio hilo alikuwepo pia Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Willium Vangimembe Lukuvi ambaye aliwapongeza Jumuiya ya vijana mkoa wa Iringa chini ya uongozi wa Kenani Kihongosi kwa kushirikiana kwa karibu na wabunge wote na kuwajengea uwezo vijana kiuchumi katika Maeneo mbalimbali hapa nchini, Akasisitiza Kuenzi kazi kubwa inayofanywa na Mh Rais Dr Magufuli kwa vijana amesema Mh Rais anawapenda vijana na anawaamini ndio mana katika Uteuzi wake nafasi nyingi amewapa vijana hivyo Vijana tunawajibu wa Kufanya Kazi na kuwa wazalendo kwa Taifa Letu
Kwa upande wa Viongozi wa serikali salamu zilitolewa na Mheshimiwa mkuu wa wilaya kilolo Bi Asia Abdallah na kumhakikishia mwenyekiti wa UVCCM Taifa Komred Kheri D James utekelezaji wa ilani unaendelea vizuri na kwa kasi kubwa pia ushirikiano baina umoja wa vijana mkoa a iringa na Serikali ni mkubwa na wenye nidhamu ya hali ya juu Alisisitiza vijana kufanya kazi kwa bidii ili kujiimarisha kiuchumi na kumuunga mkono Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Dr John Pombe Magufili kwa kufanya Kazi.
Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Komred Kheri D Jamesbalitembelea chuo cha umoja wa vijana wa ihemi kilichopo mkoani iringa ambapo kipo katika maboresho makubwa na kuahidi kuhakikisha katika uongozi wake anakifufua chuo hicho ambapo viongozi wengi wa serikali na Chama wamepikwa katika chuo na kuahidi kumuenzi mwl nyerere kwa ujenzi wa chuo na kuziishi ndoto zake, pia kuanzisha program mbalimbali zitakazo wainua Vijana kiuchumi na kuhakikisha Tunakukuwa na Taifa la Kujitegemea.
Katika mkutano huo ulihudhuriwa na KATIBU wa CCM Mkoa wa Iringa Komred Christopher Magala, Mnec Theresia Mtewele, Mwenezi wa Mkoa Wa Iringa, Wenyeviti wa CCM wilaya zote za Mkoa wa Iringa , Wenyeviti wa UVCCM Wilaya zote Mkoa wa Iringa, Kamati za siasa za wilaya zote za Mkoa wa Iringa, Sekretarieti za wilaya zote za Mkoa wa Iringa, Naibu Meya Manispaa ya Iringa na Madiwani Pamoja na Mkurugenzi wa Iringa DC
HESHIMA! Mwenyekiti wa UVCCM TAIFA Ndg Kheri James akipokelewa na kuvishwa Skafu ya Heshima
Ndg Kheri James (MCC) akisisitiza jambo mbele ya viongozi kutoka Wilaya zote za Mkoa wa Iringa
UKARIMU! Mwenyekiti wa UVCCM TAIFA Ndg Kheri James akifurahia jambo na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Willium Lukuvi aliyeungana na UVCCM Iringa kumpokea Ndg Kheri James
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM TAIFA kutokea Mkoa wa Iringa Ndg Salim Abri "Asas" akizungumza na Vijana wa Iringa
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (Viti 15 Bara) Bi. Theresia Mtewele akizungumza na Vijana
Ndg Kheri James akiwakabidhi vifaa vya michezo Viongozi wa Wilaya ya Mufindi
ASANTENI SANA! Viongozi wa UVCCM Wilaya ya Iringa Vijijini wakipokea vifaa vya michezo
Imeandaliwa na:
Sufiani Omary
Katibu Hamasa na Chipukizi UVCCM
Mkoa wa Iringa
No comments