Breaking News

ROSE ROBERT MANUMBA AMUWAKILISHA M/KITI UVCCM TAIFA KUFUNGA KAMBI YA VIJANA BUSEGA- SIMIYU





Leo Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Ndg. Rose Robert Manumba amefunga rasmi kambi ya vijana lililofanyika wilayani Busega Mkoa wa Simiyu kama Mgeni Rasmi akimuwakilisha Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Ndg. Kheri James. 

Ndugu Manumba Ametoa Salamu za Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Ndg. Kheri James Kwamba anaendelea kuwakumbusha vijana kuwa ndio nguvu kazi ya Taifa na tuendelee kupendana na kusaidiana lakini kubwa zaidi tufanye kazi kwa umoja na ushirikiano kwaajili ya maendeleo ya Taifa letu huku tukiendelea kusapoti Serikali ya Chama Cha Mapinduzi.

Ndugu M/Kiti wetu Mpendwa Kheri James amewasa na kuwasisitiza tufanye kazi kwa Bidii,Tuwe Waadilifu, Wazalendo kwa Chama na Taifa letu kwani sisi Vijana ndo Askari na walinzi wa Taifa letu Mama Tanzania. 

Ndg. Rose Manumba amewaasa vijana hao kutumia mafunzo ya Uongozi na Uzalendo waliyoyapata kwa kuwa mabalozi wazuri wa kukisemea na kutetea Chama cha Mapinduzi hasa tunapoelekea kwenye chaguzi za Serikali za Mtaa nakuhakikisha ushindi unapatikana kwa Chama ili kuunda Serikali ya Chama Kuanzia ngazi za Vijiji. 

Pia sisi vijana wa Chama cha Mapinduzi tuendelee kuunga mkono Juhudi za Mhe. Rais Dr. John Pombe Magufuli Kama vijana tuchukie rushwa na ufisadi na tuwe mstari wa mbele kuitumikia nchi kwa kushirikiana na Viongozi wa Chama na Serikali kwa ujenzi wa Taifa letu.

Manumba Amewaelekeza Makatibu wa Wilaya na Kata kuhakikisha vijana Wote wanapata Mikopo isiyo na riba kutoka katika Halmashauri kupitia katika vikundi mbalimbali ili waweze kupata mikopo kutoka Halmashauri na kujiongozea Kipato na kukuza uchumi wao na Taifa kwa Ujumla. 

Ndg. Manumba, amewakumbusha vijana kwamba tupo kwenye kipindi cha maadhimisho ya miaka 42 ya CCM na hivyo tuiishi kwa kuzingatia kauli mbiu inayosema Kazi ni kipimo cha Utu, Tuchape Kazi, tuulinde Uhuru na Utaifa Wetu

Imetolewa na: 
Idara ya Habari na Mawasiliano Busega Simiyu Tanzania

No comments