Breaking News

RAIS MAGUFULI ATEKELEZA AHADI YAKE YA MILIONI 200 NDANI YA MASAA 24

Mwenyekiti Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi- CCM Ndugu Dkt John P. J. Magufuli ndani ya saa ishirini na nne (24) ametekeleza ahadi yake ya kutoa kiasi cha shilingi milioni 200 kwa kampuni ya Africa Media Group inayomiliki kituo cha Channel ten na Magic Fm kwa ajili ununuzi wa vifaa lengo likiwa ni kuboresha utendaji kazi wa kampuni hiyo.

Fedha hizo zilizoahidiwa na Mwenyekiti Dk .J. P. Magufuli zimekabidhiwa na katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Ndugu Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga kwa niaba ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Dk. Bashiru Ally. 

Akizungumza baada ya kukabidhi hundi hiyo yenye thamani ya shilingi milioni 200 Ndugu. Kanali Mstaafu Lubinga amesema fedha hizo zimetolewa na Chama Cha Mapinduzi ili kutimiza lengo la Mwenyekiti wa CCM Taifa Dk. John Magufuli la kuona Kampuni ya Africa Media Group ltd kupitia vituo inavyoviendesha yaani CHANNEL TEN, MAGIC FM na vinginevyo, vinakuwa bora na kwa hadhi ya kimataifa.

Kanali Mstaafu Lubinga amewaambia Wafanyakazi wa AMGL pamoja na uongozi, kwamba ni matumaini ya mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Dk Magufuli kwamba fedha zilizotolewa na Chama zitatumika kama ilivyokusudiwa yaani kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya kuboreshea matangazo na si vinginevyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa AMGL Ndugu Jaffar Haniu licha ya kushukuru kwa msaada huo ameahidi kuzitumia fedha hizo kama ilivyokusudiwa bila ubadhilifu lakini pia amemuomba Mwenyekiti wa CCM Dk. Magufuli kuendelea kuisaidia kampuni hiyo pindi atakapoombwa.

Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais DK.John Magufuli alitumia siku ya maadhimisho ya miaka 42 ya kuzaliwa kwa chama cha CCM kutembelea Kampuni ya AMGL ambayo kwa sasa inamilikiwa na CCM ambapo aliahidi kutoa fedha hizo baada ya kusikiliza kilio cha wafanyakazi ikiwemo uchakazu wa vifaa. #KilichoBoraKabisa

No comments