Breaking News

OPARESHENI BENDERA YASHIKA KASI WILAYANI TEMEKE, VIJANA KUTOKA ZANZIBAR WANOGESHA "HAMASA NDIO UHAI WA JUMUIYA

Ziara ya Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Taifa kukagua Vikundi vya Hamasa Mkoa wa Daresalaam

Wilaya ya TEMEKE

Oparesheni Bendera yaendelea kushika kasi mkoa wa dar es salaam

Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM TAIFA ndugu Hassan Bomboko* ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kuvitambua Vikundi vya hamasa kama sehemu ya kurejesha Uhai wa jumuiya leo ameendelea na zoezi hilo sambamba na kukabidhi na kusimika bendera kwa mabalozi wa ccm wilaya yaTemeke kata ya Chamazi

Aidha mkuu wa idara aliambatana na Mwenyekiti wa Vijana Mkoa wa Darasalaam Mussa Ramadhani Kilakala, Katibu wa vijana mkoa ndugu Saidi Yasini pamoja mjumbe wa baraza kuu la vijana Taifa ndugu Gwanta Alex Mwakijungu, ambao kwa pamoja walitumia wasahaa huo kuwanasihii na kuwakumbusha vijana wa mkoa wa daresalama juu ya Ujenzi wa Jumuiya na Chama cha Mapinduzi kwa Ujumlaa

Akimkaribisha Mkuu wa idara ya hamasa Mwenyekiti wa Vijana Mkao wa Daresalaam Ndugu Mussa Kilakala amewataka vijana wa temeke kuhakikisha wanajipanga vyema na Uchaguzi ujao wa serikali za mitaa na Vijiji na vitongo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanapambana kurejesha maeneo yote ambayo yako upinzani kwa sasa, lakini pia Mwenyekiti Mussa amemsisitiza mkuu wa idara ajaribu kuondoa matabaka baina ya vijana wa ccm, na kuwakumbuka vijana wa mkoa wa daresalama wanaokitumikia chama muda wote katika fursa mbalimbali za ajira zinazojitokeza 

Nae mbaraza wa wa mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Gwanta Alex Mwakijungu alimshukuru Mkuu waidara kwa kazi nzuri anayoifanya ya ujenzi wa jumuiya lakini wasiishie kuvitambua vikundi vya hamasa bali wahakikishe wanatengeneza utaratibu mzuri kwa vijana hawa kuweza kukitumikia chama kwa tija na manufaa baada ya shughuli za chama

Katika ziara hiyo pia ilihudhuriwa na Wajumbe wa baraza kutoka Mkoa wa Njombe Ndg Omega Thobias na Pwani Ndg Ramadhani Mlao ambao kwa pamoja walipata nafasi ya kupanda mti kama sehemu ya kumbukumbu na inayolenga kuonyesha Umoja na Mshikamano baina ya vijana wote Nchi Nzima. 

Imetolewa na
Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM TAIFA

MATUKIO KATIKA PICHA






No comments