Breaking News

KAMPENI YA "BINTI ITAMBUE THAMANI YAKO" YAFUNGULIWA RASMI WILAYANI BUSEGA-SIMIYU NA DC TANO MWERA

Mkuu wa Wilaya ya Busega Mkoani SIMIYU afungua rasmi Kampeni ya Binti itambue thamani yako akiwa ameambatana na Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana Tanzania ndugu Rose Robert Manumba na ameweza kuitambulisha rasmi Kampeni hiyo iliyozinduliwa Jijijini Dar Es Salam pia Mwaka Jana Mwishoni. 

Aidha Mkuu Wa Wilaya Mhe. Tano Mwera ameweza kuwahasa Mabinti hao kutambua thamani zao kwa kuzingatia elimu na kusoma kwa bidii ili waweze kufikia malengo na ndoto zao katika maisha.

Amewaasa mabinti hao kujichunga na kuepukana na vishawishi ambavyo vinaweza kukwamisha maendeleo yao kimasomo na kupelekea kushindwa kufikia malengo hivyo kutumia nafasi hiyo ya elimu bure vizuri kwa kusoma kwa bidii na hatimae kufikia malengo kuja kulitumikia Taifa Pamoja na Familia zao. 

Katika uzinduzi huo Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM Taifa na Mwanasheria Ndg. Rose Manumba pia amewaasa mabinti hao kusoma kwa bidii wakitambua kwamba elimu hiyo wanayoipata ni kwaajili ya faida za Jamii zao na Taifa la Tanzania kwa Ujumla. Watambue Kwamba Taifa lina matarajio Makubwa Kwamba ujuzi wa fani mbalimbali wanaoupata katika elimu zao utatumika kwaajili ya ujenzi wa Taifa letu. 

Ndugu Manumba amesisitiza kuwa kutambua thamani yako kama Binti wa kitanzania ni pamoja na kulinda Maadili na Tamaduni zetu nzuri za Kitanzania kama kuzingatia Mavazi ya Stara Kwani Kujistiri sio Ushamba na huletea heshima na utu Kama Binti wa Tanzania..

Amehitimisha Ndg. Manumba kwa kusema kutambua thamani yako Kama Binti ni pamoja na Kutambua haki zako za msingi kama kushiriki katika Maendeleo ya Ujenzi wa Taifa lako, kupata elimu, kushiriki katika vikao vya maamuzi kwa nafasi yako, kuwa kiongozi na kumiliki uchumi mkubwa na kuendelea kupinga nyanja zote za unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya mtoto wa kike. 

Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Simiyu Ndg. Getrude Mazengo amewaasa mabinti hao kujifunza kupambana na changamoto na hasa changamoto ya rushwa ya ngono inayowapelekea kushindwa kufikia malengo na ndoto zao kwa kupata madhara kama mimba za utotoni, magonjwa na hata kufeli kwenye masomo yao. Amewasisitiza kutoa taarifa katika vyombo husika vya Serikali kama Dawati la Jinsia pale wanapokutana na changamoto hizo. 

Imetolewa na:
Idara ya Habari na Mawasiliano Busega Simiyu

No comments