Breaking News

UVCCM YAMLIPUA SUMAYE YATAKA KABLA YA KUMKOSOA RAIS MAGUFULI ATAJE UADILIFU WAKE


Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM TAIFA ndg Hassan Bomboko amewaeleza vijana wa ccm Wilaya ya Geita kwamba "Sumaye ni Mpinzani dhaifu na goigoi Mwenye Uchu wa Madaraka, Katika historia ya nchi yetu sumaye ndio waziri mkuu aliyedumu kwa vipindi viwili vya miaka kumi naweza kuwaambia watanzania wampuuze mzee sumaye kwani records za utendaji wake zinaonyesha ndio waziri mkuu Dhaifu na goigoi kuwahi kutokeka" 

Ndg hassan Bomboko aliyasema hayo katika hotuba yake wakati Akifunga kambi la vijana wilaya ya Geita.:

Juzi Tulimsikia Mzee Fadrick Turway Sumaye aliyekuwa waziri mkuu mstasfu akisoma maazimio ya kikao chao cha kanda cha CHADEMA

Hotuba ya Sumaye ilijaa sauti yenye kutia hurumaa ikionyesha ni namna gani upinzani wa tanzania Hauna stamina na hauna pumzi ya kuikabili Chama Tawala CCM

Upinzani huu wenye kuongozwa na mtu goigoi kama Sumaye hauwezi kutoa Chama Mbadala kitakachoweza kuja na sera, Fikra na Maono ya Kukabiliana na Ukubwa wa CCM katika Sera na ILANI

CCM chini ya Mwenyekiti Dr John Pombe Magufuli Imeinyima Upinzani wa Tanzania Agenda Mpya, zilizokuwa agenda na Maono yao Dr Magufuli ameyatafsiri kwa vitendo katika Utekelezaji wa Ilani ya CCM 2015 - 2020

Kutapatapa kwa Sumaye na wenzie akina zitto kabwe ni dalili moja wapo ya Kifilisika kwa upinzani katika Agenda zote walizowahi kuzibeba na kuzifanya kuwa sera, Dr John Magufuli ametekeleza Mambo yote waliokuwa wakiyalalamikia

UVCCM tuendelee kusimaa imara na kuendelea na wajibu wetu namba moja wa kukilinda Chama cha Mapinduzi, Serikali ya Chama cha Mapinduzi na viongozi wake huo ndio wajibu wa vijana.

Vijana tusikae kimya tutoke tukaeleze utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi tueleze Mambo makubwa ya maendeleo yanayofanywa na serikali ya Awamu ya tano.

Ni fedheha kwa vijana wa ccm kushinda mitandaoni kushambulia viongozi wao badala ya kueleza kasi ya Utekelezaji wa Ilani unaofanywa na Rais Magufuli

Vijana wa CCM tumekuwa kimya tukiwaacha wapotoshaji akina zitto kabwe kuendelea kutumika na vibara kupandikiza chuki kwa watanzania dhidi ya serikali yao inayowaletea maendeleo

Zitto Kabwe hana Uhalali wa kisiasa "Moral authority" kwani ni mwanasiasa ndumi la kuili, aliye na record ya usaliti katika vyama vyote alivyowahi kupitia "Ifahamike alifukuzwa chadema kwa tuhuma za usaliti wa kutaka kumpindua Mwenyekiti wake mbowe na hata ACT alifanya mapinduzi kwa waanzilishi waasisi wa chama hicho" hivyo mtu kaliba ya zitto kabwe sio aina ya mwanasiasa wa kuaminiwa na umma.

Zitto anahaha kukwamisha jitihada za maendeleo vijana wa ccm fanyeni na nyie jitihada za kumkwamisha yeye kwa sasa amekimbia jimbo lake nanyi tumieni mfumo uleule kukabiliana na msaliti wa Taifa letu

Nitumie hadhara hii kurejea kusema tena UVCCM haitomfumbia macho Mpinzani yoyote wa njee na ndani ya Chama cha mapinduzi

Niwatake tena wenye makundi mbalimbali ndani ya Jumuiya ya vijana na ndani ya Chama cha mapinduzi waache mara moja Vinginevyo hatutasita kuwawajibisha

Wanaotengeneza Mitandao ya Uraisi nao waache mara moja wao na magenge yao wakatafute kazi nyingine ya kufanya CCM hatuna agenda ya kutafuta Mgombea uraisi 2020 Tunaye dr John pombe magufuli

Kama ni mbunge fanya kazi ya ubunge uliopewa na wananchi, kama ni Mkuu wa wilaya, mkuu wa mkoa fanya kazi ya uliyopewa achana na mitandao ya wasaka madaraka, kama ni Waziri au naibu waziri pia ni Marufuku kuanza kufanya harakati za kutafuta madara wajibu wenu kwa sasa ni Kumsaidia Raisi katika Utekelezaji wa Ilani ya CCM 2015 - 2020

Mwisho niwatake vijana wa ccm Nchi nzima tujipange na tujiandae kwa Uchaguzi ujao ngazi ya serikali za Mitaa, Vitongoji na vijiji.
Mapokezi ya Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi Ndg Hassan Bomboko Wilayani Geita
Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Taifa Ndg Hassan Bomboko akisalimiana na Wazee waasisi wa CCM wa Wilaya ya Geita
"HESHIMA KWA KIONGOZI"

Ndg Hassan Bomboko akimkabidhi cheti moja wa Chipukizi Wilayani Geita

No comments