Breaking News

FAIDA ZA KILIMO CHA MBOGA MBOGA KWA FAMILIA


Katika maisha ya familia ni lazima kujituma katika mambo yanayowezekana angalau kupunguza gharama za maisha yanayoikabili familia. Leo tumeona ni vyema tukafahamu mambo muhimu tunayoyapuuza, lakini yanaweza kusaidia kupunguza ukali wa maisha.

Kilimo cha mboga mboga ndani ya familia ni hatua pekee ya kupunguza ukali wa maisha na kuepuka gharama zisizo za msingi ndani ya familia. Hapa nazunguzia kwa wale wenye maeneo binafsi na wanaishi mjini au hata vijijini, tumia eneo ulilonalo kulima hata matuta mawili tu ya mboga mboga; kwamfano nyanya, sukuma wiki, mchicha na kadhalika.

Tumia nafasi ulionayo hata kama ni kutumia makopo kama mauwa, panga miche yako ya nyanya na sukuma wiki au mchicha, ili kuokoa pesa yako kwenda sokoni kila siku. Kuna baadhi ya mboga mboga huchukuwa siku chache kuota na kukua; kwamfano mchicha huchukuwa siku chache tayari unavunwa.

Kuwa na bustani ndogo ya mboga mboga nyumbani haikushushi hadhi hata kama wewe ni tajiri, unaweza kumpa maelekezo msaidizi wako pale nyumbani akapanda hata matuta mawili tuu ya karoti au nyanya, endapo wewe uko bize.

Bustani ya mboga mboga katika ngazi ya familia sio tuu inasaidia kupunguza matumizi bari inakupatia uzoefu wa kujituma katika kazi. Kwamfano wenzetu wa majuu hutenga muda wao wa jioni na asubuhi sana kufanya kitu katika bustani zao aidha za maua au mboga mboga. Kama bado hukujua utamu wa bustani, basi anza leo.

No comments