Breaking News

UVCCM DAR ES SALAAM YACHIMBUA FURSA ZA VIJANA KWA MKURUGENZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM.

———————————————
Dar es Salaam, Tanzania.

Viongozi wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam wakiongozwa na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Ndg. Musa Kilakala jana walifanya ziara katika ofisi ya Mkurugenzi wa jiji la Dar es Salaam.

Ziara hiyo iliyokuwa na lengo kubwa la kutaka kujua juu ya mikopo inayotolewa kwa vijana na kufahamu fursa mbalimbali za vijana zinazopatikana katika ofisi hiyo.

Sambamba na hilo walijadiliana na Mkurugenzi wa jiji juu ya namna bora ya kutatua changamoto zinazowakabili vijana wanaoendesha pikipiki maarufu kwa jina la bodaboda wanaofanya shughuli zao katika Mkoa huo.

Akizungumza wakati wa kikao hiko Mkurugenzi wa jiji la Dar es Salaam Bi. Spola Liana aliwaahidi viongozi hao kuwapa ushirikiano wa kutosha na kuwaahidi kuwa nao bega kwa bega kwa maslahi ya Vijana wa Mkoa huo.

Pia aliwataka viongozi hao kuwa wepesi wanapoona kuna mambo yanaenda ndivyo sivyo sambamba na kuwataka kuwa walinzi wanapoona kuna vitendo vya rushwa vinatokea na kuripoti katika eneo husika.

Mwisho Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam Ndg. Musa Kilakala alimshukuru Mkurugenzi huyo kwa kuwapokea na kujadili kwa kina namna bora ya kutatua changamoto mbalimbali za vijana wa Mkoa wa Dar es Salaam.

#Tukutane Kazini.

No comments