Breaking News

POLEPOLE AWAIVISHA ITIKADI, IMANI YA CCM VIONGOZI WA UVCCM MAKAO MAKUU

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Humphrey Polepole leo tarehe 01/11/2018 amehudhuria Semina ya Mafunzo ya Uongozi na kujenga uwezo wa Taasisi ya UVCCM Makao Makuu yanayofanyika katika Chuo cha Usafirishaji (NIT) jijini Dar es Salaam kwa siku tatu(3) na kutoa mafunzo kuhusu Itikadi na Uenezi ya CCM.

Katika semina hiyo ya Uongozi iliyohusisha Watumishi wa Makao Makuu ya UVCCM Taifa na Viongozi wa Mkoa wa Dar Es Salaam Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Ndugu Polepole ambaye ndiye Mkuu wa Mafunzo ya Chama, alieleza umuhimu wa mafunzo kwa Viongozi, watendaji na Vijana wote wa CCM. Lakini pia Ndugu Humphrey Polepole alieleza kazi kubwa ya kuleta maendeleo inayofanywa na Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.

Aidha, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Humphrey Polepole aliutaka Umoja wa Vijana wa CCM kuendelea kukilinda na kukitetea Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais Dkt John Pombe Magufuli pamoja na kueneza maendeleo makubwa yanayofanywa na Serikali ya awamu ya tano chini.

Imetolewa na;
Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Taifa.
UVCCM Mpya.
CCM Mpya, Tanzania Mpya.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndg Polepole akisalimiana na Viongozi wa UVCCM mara baada ya kuwasili Chuo cha Usafirishaji (NIT) 
TUPO KAZINI!! 
Wanasemina wakiendelea na Mafunzo

No comments