Breaking News

MZEE MANGULA AHIMIZA VIJANA KUZINGATIA MAADILI NA NIDHAMU, ASISITIZA UADILIFU KUWA KIPIMO CHA UONGOZI KWENYE CHAMA NA SERIKALI

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Bara Ndugu Philip Mangula leo amehudhuria Semina ya Mafunzo ya Uongozi na kujenga uwezo kwa watumishi wa Taasisi ya UVCCM Makao Makuu na Mkoa wa Dar Es Salaam inayofanyika katika Chuo cha Usafirishaji (NIT) kilichopo Mabibo jijini Dar es Salaam.

Ikiwa leo ni siku ya pili ya Semina hiyo kati ya siku tatu(3) Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara Ndugu Philip Mangula amepata wasaa wa kutoa mada ya Maadili ya Uongozi na kuwata Vijana wa Umoja wa Vijana wa CCM kufuata Miiko ya Uongozi ya Chama cha Mapinduzi.

Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Ndugu Mangula amewataka Viongozi kuwa Waadilifu kwani ndio msingi wa Kiongozi na Mwanachama bora, “Viongozi wengi wamekosa Uadilifu kutokana na kukosa hofu ya Mungu, Viongozi ninyi kuweni wacha Mungu ili kuwa wanyoofu wa tabia na Waadilifu”.

Aidha, Katika Semina hiyo Makamu Mwenyekiti wa CCM Ndugu Philip Mangula alitoa ufafanuzi kuhusu Azimio la Zanzibar’ na kueleza ukweli ya kwamba hakuna kitu kama hicho bali kuna ‘Uamuzi wa Zanzibar’.
Makamu Mwenyekiti wa CCM TAIFA (Bara) Mzee Philip Mangula akikagua ufundishaji wa wanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji
CCM Mpya TANZANIA Mpya+

Imetolewa na;
Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Taifa.
UVCCM Mpya.
CCM Mpya, Tanzania Mpya.

No comments