Breaking News

POLEPOLE AFUNGUA AWAMU YA PILI YA MAFUNZO YA KIMKAKATI KWA VIONGOZI, WATENDAJI UVCCM

Katibu wa NEC- Itikadi na Uenezi Chama Cha Mapinduzi Ndg Humphrey Polepole amefungua awamu ya pili ya Mafunzo ya Kimkakati kwa Viongozi na Watendaji wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi inayoendelea Mkoan Dodoma.

Akizungumza na Viongozi hao Ndg Humphrey Polepole ametoa Mafunzo ya Itikadi na Siasa na Uenezi katika Chama cha Mapinduzi.

Awali Ndg Polepole ameupongeza Uongozi wa Umoja wa Vijana wa CCM kwa kutambua umuhimu wa mafunzo hayo yatayo saidia kuwajengea Uwezo Viongozi hao.

"Mafunzo haya yatawajenga kuwa zaid na Maarifa mapya kwa Sababu hakuna mtu mwingine wa Kumpatia mafunzo haya kwa Chama isipokuwa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi kwa Sababu nyinyi mpo leo na ndio Viongozi wa kesho" Alisema Ndg Polepole.

Aidha, ameendelea kuwasisitiza Viongozi hao kuendelea kumuunga Mkono, Kuyasemea na Kuyasimamia mambo yote anayoyafanya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa Maslahi mapana ya Taifa.

#TukutaneKazini
Viongozi wa UVCCM wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti UVCCM TAIFA Bi. Tabia Maulid Mwita wakimpokea Katibu wa NEC- Itikadi na Uenezi CCM Ndg Humphrey Polepole mara baada ya kuwasili Ukumbi wa Semina.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania ya Chama cha Mapinduzi Ndugu Erasto Sima akisisitiza jambo kwa Viongozi wa UVCCM.
Viongozi wakuu wakiongoza kuimba nyimbo za Hamasa kwenye Semina ya Viongozi na Watendaji wa UVCCM

No comments