NAIBU WAZIRI ULEGA, HUSSEIN BASHE, MBONI MHITA WATOA ELIMU MAARIFA KWA VIONGOZI NA WATENDAJI UVCCM
Katika muendelezo wa mafunzo ya Kimkakati kwa watendaji wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mikoa ya Tanzania Bara na Visiwani,Wabunge watatu ambao pia ni matunda ya UVCCM wameshiriki katika kutoa mafunzo.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mhe Abdalla Ulega amezungumza na kutoa hamasa kwa Viongozi namna ya kuimarisha utendaji kazi utakaoendelea kukipa nguvu Chama Cha Mapinduzi katika kila Mkoa.
Naye Mbunge wa Jimbo la Nzega Mhe Hussein Bashe ameshiriki kwa kuwasilisha mada ya Kujitegemea kiuchumi ambapo aliainisha mbinu mbalimbali sahihi za kuinua taasisi kiuchumi.
Aidha Mbunge wa Jimbo la Handeni Vijijini Mhe Mboni Mhita ameshiriki kwa kuwapa wana semina namna bora ya kutimiza majukumu yao kwa kutanguliza ubunifu.
#TukutaneKazini
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalla Ulega akiwasilisha mada kwenye semina ya viongozi na watendaji wa UVCCM
Mbunge wa Jimbo la Nzega Mhe. Hussein Bashe akisisitiza jambo kwa Viongozi wa UVCCM Jijini Dodoma
Mbunge wa Jimbo la Handeni Vijijini na Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa UVCCM TAIFA Mhe. Mboni Mhita akitoa salamu na somo lake kwa viongozi wa UVCCM
No comments