Breaking News

UVCCM RUVUMA WAFANYA UKAGUZI ENEO LAO KWA AJILI YA KUANZA UJENZI WA NYUMBA YA KATIBU WA UVCCM NA UJENZI WA HOSTEL

Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Ruvuma Ndg Raymund Mhenga akitoa maelekezo mara baada ya kukagua maeneo ya kufanyia ujenzi wa hostel na nyumba 
Umoja wa Vijana Mkoa wa Ruvuma leo wametembelea eneo lao lililopo kata ya Lizaboni,Mtaa wa Londoni. Kamati ya utekelezaji ya Uvccm Mkoa wakiongozwa na Mwenyekiti wa Uvccm Mkoa wa Ruvuma Comrade Raymund Mhenga waliambatana na Katibu wa Uvccm Wilaya ya Songea Mjini,Mwenyekiti wa Uvccm Kata ya Lizaboni,Diwani wa kata ya lizaboni,Mwenezi wa CCM Wilaya ya Songea Mjini Ndugu Luanda,ambaye Mwaka 1988 wakati Uvccm wakipewa eneo hilo lilikuwa likitumika na Chama cha FRELIMO alikuwa Mjumbe wa kamati ya Utekelezaji wa Uvccm Mkoa Songea Manispaa. 

Baada ya Ziara katika eneo hilo lenye hekari zaidi ya 6, Kamati ya utekelezaji ya Uvccm Mkoa wametoa maelekezo kwamba watu wote ambao wameingilia eneo hilo kwa kulima na matumizi mengine wasitishe mara moja,lakini Pia wameiagiza Serikali ya Mtaa na Kata kuhakikisha wanawaasa wananchi wote kutokuingilia eneo hilo la UVCCM ambalo linamilikiwa kihalali na ndani ya miezi minne Ujenzi wa Nyumba mbili za Watumishi wa Jumuia na Hostel utaanza.Na kwa kuanzia mapema kuanzia wiki Ijayo UVCCM watazungushia ujio wa Nguzo za zege kwa ajili ya kuweka mipaka inayoeleweka kihalali. 

Mwenyekiti alimaliza kwa kuwashukuru Wananchi wa eneo hilo,viongozi wa serikali wakiongozwa na Diwani na Viongozi wote wa Vijana kwa kusimamia maeneo hayo. 

Viva Vijana Viva# Tukutane Kazini# 
Imetolewa na
Ndg Sikitiko Abdul Komba
Katibu Hamasa na Chipukizi UVCCM (M) RUVUMA

No comments