Breaking News

OPERESHENI BENDERA YATUA WILAYANI KIGAMBONI "HAMASA NDIO UHAI WA JUMUIYA"

Ziara ya Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Taifa kukagua Vikundi vya Hamasa Mkoa wa Dar es Salaam Wilaya ya Kigamboni.

Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM TAIFA ndug Hassan Bomboko* leo jumatatu ameendelea na oparesheni Bendera katika kata ya Kigamboni , Wilaya ya kigamboni

Katika ziara hiyo ameendelea na zoezi la kuvitambua na kuvijengea uwezo Vikundi vya hamasa katika ngazi ya Kata kama sehemu ya Kuimarisha uhai wa jumuiya 

Mkuu wa idara amewaagiza vijana Wilaya ya Kigamboni Kuendelea kusimama imara katika kukisemea na kukihami Chama Cha Mapinduzi ikiwa ni sehemu ya kutekeleza wajibu na majukumu ya kijana wa CCM katika Ujenzi wa Chama na Taifa 

Aidha Ndg Bomboko ametembelea nyumba mbali mbali za mabolozi wa CCM kama sehemu ya kurejesha hari na kuwatia moyo mabalozi wa CCM wilaya ya Kigamboni zoezi lililoenda sambamba na kukabidhi na kusimika bendera katika nyumba za viongozi hao wa Shina

"Ndugu zangu nimepita wilaya mbili za mkoa wa dsm na leo nipo hapa Kigamboni, kubwa nimekuja na mpango wa kuitumia Hamasa kama njia ya kurejesha Uhai katika Jumuiya yetu, Nitoe wito kwa viongozi wenzangu tuendelee kukipigania Chama na kukiletea ushindi katika uchaguzi wa serikali za mitaa vitongoni na vijiji uliombioni na Tujiandae pia kwa Uchaguzi mkuu 2020" alisema Ndg Bomboko 

"Mwisho nitoe salamu za Mwenyekiti wa Vijana Taifa Comrade Kheri Denice James mwenyekiti amesisitiza vijana tuendele kushirikiana na kushikamana, umoja wetu ndio ushindi wa wetu na ushindi wetu ndio ushindi wa Chama Cha Mapinduzi, bila upendo baina yetu shughuli hizi za ujenzi wa Chama chetu kupitia Jumuiya yetu hazitakuwa na tija, ni wito wa Mwenyekiti wetu kwa vijana Nchii nzima Kuwa wamoja." Aliongeza Ndg Bomboko wakati anawahutiba vijana wa wilaya ya Kigamboni

Imetolewa na
Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM TAIFA

MATUKIO KATIKA PICHA










No comments