MKUTANO WA 13 WA BARAZA LA WAWAKILISHI SMZ KUANZA FEBRUARI 06
Mkutano wa kumi na tatu wa Baraza la tisa la Wawakilishi unatarajiwa kuanza febuari 6 ambapo jumla ya miswada miwili inarajiwa kusomwa tena kwa mara ya pili.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari katika ukumbi wa Baraza hilo Chukwani Nnje kidogo ya Mji wa Zanzibar ,kuhusiana na Mkutano huo katibu wa Baraza la Wawakilishi zanzibar Raya Issa Mselem amesema miongoni mwa miswada hiyo itayosomwa kwa mara ya pili ni Mswada wa sheria ya kuazishwa wakala wa serikali wa huduma za matrekta na zana za kilimo.
Alisema mswada mwengine ni Mswada wa sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali ya Mwaka 2018 na mambo mengine yanayohusiana na hayo.
Katibu Raya alisema Mkutano huo pia Utawasilishwa Ripoti za kamati za kudumu za Baraza la wawakilishi kwa mwaka 2018/19 pamoja na Mwelekeo wa mpango wa taifa. Katika mkutano huo jumla ya maswali 146 yanatarajiwa kuulizwa na wajumbe wa baraza la Wawakilishi na kujibiwa kutoka kwa serikali.
Alisema katika mkutano huo pia kutawasilishwa ripoti teule ya kuchunguza majengo ya skuli 19 za sekondari za Zanzibar pamoja na Taarifa ya serikali kuhusu hoja ya Mjumbe kuliomba Baraza kutoa maadhimio ya kushughulikiwa vifaa tiba vya Hospitali ya Abdallah Mzee ya Mkoa Pemba.
No comments