Breaking News

UPASUAJI WA KUONDOA VIVIMBE KWENYE MISHIPA YA DAMU KWENYE UBONGO WAFANYIKA KWA MARA YA KWANZA MOI

Profesa Philip Stieg kutoka Chuo Kikuu cha Weill Cornell cha Marekani, akiongoza upasuaji wa mgojwa aliyepata kiharusi. Kuanzia kulia ni Dkt. Japhet Ngerageza, Dkt. Laurent Lemeri na Dkt. Alpha King'omela. (PICHA NA KHAMISI MUSSA).

NA KHAMISI MUSSA
Leo upasuaji wa kuzibua vivimbe kwenye Ubongo umefanyika kwa mara ya kwanza hapa MOI kwa mafanikio makubwa. Upasuaji huo umefanyika kwa masaa 5 ambapo jopo la madaktari bingwa waliofanya upasuaji huo limeongozwa na Profesa Philip Stieg kutoka Chuo Kikuu cha Weill Cornell cha Marekani. Upasuaji huo umefanywa kwa mgonjwa aliyepata kiharusi. Awali wagonjwa walilazimika kwenda nje ya nchi kwa matibabu haya kwa gharama kubwa.

No comments