Breaking News

UJERUMANI YAMPONGEZA RAIS MAGUFULI KUPAMBANA NA RUSHWA- BALOZI WAECHTER

Na Judith Mhina – MAELEZO

Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Dkt Detlef Waechter amempongeza Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli kwa kufanikiwa kupambana na rushwa nchin Tanzania na kupata mafanikio makubwa ndani ya kipindi kifupi.

Hayo amesema Balozi Waechter alipofanya mahojiano na Idara ya Habari MAELEZO mapema jana katika hoteli ya Hyatt Regency The Kilimanjaro Dar-es-salaam Kempinski katika barabara ya Sokoine Jijini Dar-es –salaam.

Akielezea jinsi rushwa ilivyoota mizizi sehemu nyingi ikiwemo Ujerumani amesema “Tatizo la rushwa sio la Tanzania peke yake, hata pale Ujerumani lipo japo si kwa kiasi kikubwa, bali kila mara serikali inapaswa kujiangalia na kuhakikisha inapambana na mfumo wa rushwa mahala popote. Ili raia wako wawe na imani na serikali yako”

Kwa dhati kabisa nampongeza Rais Magufuli kwani hali ilikuwa sio nzuri kulingana na ripoti tuliyoisikia wakati wa Mkutano wa 38 wa Bara la Afrika wa Kuthibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya miezi mawili iliyopita. Uwepo wa rushwa Tanzania ilikuwa ni eneo linalotumiwa katika kupitisha madawa hayo ambapo sasa suala hili limepungua kwa kiasi kikubwa kutokanana juhudi za Rais Magufuli.

Akielezea ubaya wa rushwa Balozi Waechter amesema kuwa matatizo ya rushwa yanarejesha nyuma maendeleo kwa kuwa watu hawapati huduma wanazostahili kwa kuwa tu kuna wengine wanatumia rushwa. Halikadhalika uwepo wa rushwa unaondoa uaminifu kutoka Taifa moja kwenda linguine au nchi moja kwenda nyingine.

Ukiangalia maeneo ambayo hayana utulivu na amani, inatokana na kushamiri kwa rushwa na kuwa na serikali ambazo hazisimamii vema huduma kwa wananchi wake. Hili ni tatizo kubwa lililokumba nchi za kiafrika ambazo raia wake kila siku wanatafuta njia ya kuelekea Ulaya.

Raia hao wanakwenda ulaya sio kwa kupenda ni kwa sababu wamekosa utulivu na amani katika nchi zao, kinachopatikana nchini kwao ni kwa ajili ya wajanja wachache wanaoweza kutoa rushwa na kuhodhi utajiri wa nchi badala ya kuhudumia umma wa nchi nzima. Amesema Balozi Waechter.

Pia Balozi Waechter ameongeza kwa kusema kuwa nimefurahishwa na Tanzania kuona umuhimu wa viwanda katika kujenga uchumi wa nchi ya Tanzania, kwani sio rahisi uwe mzalishaji wa malighafi alafu umtehgemee mtu mwingine anunue na nchi yako ipate faida. Nadhani ni uamuzi wa busara kabisa walioufanya Tanzania kuelekea katika nchi ya viwanda.

Nchi zote zilizoendelea kama Ujerumani zimefika hapo zilipo baada ya kufanya mageuzi ya hali ya juu katika suala zima la viwanda na tekinolojia, Ujerumani ipo tayari kushirikiana na Tanzania pale ambapo itahitajika katika kuendeleza juhudi za kufanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda,

Aidha mpaka sasa wapo wawekezaji kadhaa wa Ujerumani ambao wamewekeza katika masuala ya Uzalishaji cement Mfano ni kiwanda cha cement cha Tanga, Pia kuna mradi mkubwa wa kupeleka maji safi na salama katika Mji wa Kigoma ambapo maji yanatolewa katika ziwa Tanganyika kwa ajili ya matumizi ya watanzania,

Mahusiano ya Tanzania na Ujerumani ni mazuri sana na tunatarajia kuendelea kushirikiana katika masuala mbalimbali ya kijamii, kiuchumi, na kimaendeleo kwa faida ya nchi zetu mbili. Pamoja na hayo tunauhusiano wa muda mrefu sana kati ya Ujerumani na Tanzania mara tu baada ya uhuru wa Tanganyika hadi sasa.

Akielezea suala zima la nchi zote mbili kujifunza kutoka kwa mwenzake amesema Ujerumani inajifunza kitu kikubwa sana hapa Tanzania ambacho chimbuko lake ni Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere suala zima la Amani na Utulivu ambao mimi binafsi sijawahi kuuona sehemu yeyote ambayo nimeweza kuishi.

Wito wangu ni kuwa kwa kuwa mmeamua kuijenga Tanzania ya viwanda itategemea sana hali yenu ya amani na utulivu mlionao ambao sina shaka kwa kuwa ni mabingwa wa hali yote Barani Afrika na duniani nina hakika mtafanikiwa kutimiza azma yenu . Muungeni mkono Rais Dkt Magufuli mtafanikiwa.

No comments