Breaking News

MNEC NDG THERESIA MTEWELE AWATAKA VIONGOZI WILAYA YA WANGING'OMBE KUJIKITA KATIKA MISINGI YA UONGOZI BORA NA UWAJIBIKAJI, AFUNGUA SHINA JIPYA

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (MNEC) Ndugu Theresia Mtewele ameyasema hayo wakati akifungua kambi ya UVCCM Wilayani humo itakayofanyika kwa muda wa siku (3).

Kambi hiyo imehusisha Umoja wa Vijana na viongozi wengine wa Chama Cha Mapinduzi katika Wilaya ya Wangingombe kwa lengo la kuwajengea vijana uwezo kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Aidha, MNEC Ndugu Mtewele ameelekeza misingi ya uongozi bora na uwajibikaji kwa kuongeza kuwa baada ya chaguzi yoyote kinachofuata ni kubeba dhamana ya kuwatumikia waliowachagua kwa kujibu,kutoa maelezo kwa wanaowaongoza juu ya Utekelezaji na mipango ya majukumu yao kwa lengo la kuonyesha njia ya dira iliyokusudiwa na Chama Cha Mapinduzi ili waweze kupima utendaji wao na kutatua changamoto zinazowakabili. 

Pamoja na mambo mengine MNEC Ndugu Mtewele amefungua shina la Chama Cha Mapinduzi na kuwaomba viongozi kuendelea kuisemea vizuri serikali ya awamu ya tano kwa Kazi nzuri inayofanya na kuwalinda viongozi wanaopeperusha Bendera ya Chama Cha Mapinduzi wakiwemo Wabunge na Madiwani ili wafanye Kazi zao kwa Uhuru na Amani.

Katika msafara huo MNEC ameongozana na Mwenyekiti UVCCM Mkoa wa Njombe Ndugu Tweve, Kaimu Katibu UVCCM Mkoa wa Njombe Ndugu Daniel na viongozi wengine wa Chama Mkoani Njombe.

Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Wanging'ombe Ndugu Michael Nyelegeti amewataka Vijana wa Wilaya hiyo kuwa wasikivu Kwa watoa mada ili waweze kuiva kiitikadi na maarifa na hatimaye kuwa mabalozi wazuri katika kata zao. Viongozi wengine waliokuwepo ni Katibu wa CCM Wilaya ya Wanging'ombe Bi. Agness Kasela, Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji UVCCM Wilaya, viongozi wa Jumuiya zingine za Chama Cha Mapinduzi Wilaya, viongozi wa Chama Kata na baadhi ya madiwani wakiongonzwa na Mh. Vumilia.
MNEC Theresia akisikiliza michango ya wanachama mara baada ya kufungua shina la Chama cha Mapinduzi
TUKUTANE KAZINI!! Kazi yetu Kukijenga Chama na Kutatua kero za watu wetu hasa wanyonge

No comments