Breaking News

MAKAMU MWENYEKITI UVCCM TAIFA BI. TABIA MWITA AHITIMISHA SEMINA YA MAFUNZO YA UONGOZI, AWAASA VIONGOZI KUTOJISAHAU

Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Ndugu Tabia Maulid Mwita amefunga Semina ya mafunzo ya Uongozi kwa Watumishi wa UVCCM Makao Makuu na Viongozi wa Dar es Salaam iliyokuwa ikifanyika Chuo cha Usafirishaji NIT kilichopo Mabibo jijini Dar Es Salaam.

Katika semina hiyo iliyodumu kwa siku tatu Makamu Mwenyekiti Ndugu Tabia Mwita amewataka wahitimu wa mafunzo kwenda kufanyiakazi yale waliyojifunza kwa Vitendo.

Katika Semina ya mafunzo Makamu Mwenyekiti Ndugu Tabia Mwita aliwataka Viongozi kujitahidi kuonyesha imani kwa watu wanaowaongoza, “Sisi Viongozi tuonyeshe imani kwa watu tunaowaongoza na tusijisahau” alisema Ndugu Tabia.

Aidha, Kwa heshima Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Ndugu Tabia aliwashukuru Uongozi wa Chuo cha N.I.T na TEF. Pia Makamu alitoa Vyeti kwa wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi.
Makamu Mwenyekiti UVCCM TAIFA Bi. Tabia Maulid Mwita akisalimiana na Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Mzee Wilson Mukama alipowasili kwenye Semina ya Uongozi Chuo cha Taifa cha Usafirishaji
Bi. Tabia Maulid Mwita akizungumza na wanasemina 
Makamu Mwenyekiti wa UVCCM TAIFA Bi. Tabia M. Mwita akigawa vyeti kwa washiriki wa semina


Imetolewa na;
Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM TAIFA.
UVCCM Mpya. 
CCM Mpya, Tanzania Mpya.

No comments