Breaking News

KATIBU MKUU MSTAAFU WA CCM MZEE WILSON MUKAMA AWAASA VIONGOZI VIJANA "KUJIKOSOA NA KUKOSOANA KATIKA VIKAO"

Hayo yamesisitizwa leo kwenye Semina ya Uongozi iliyoandaliwa na Umoja wa Vijana wa CCM Makao Makuu katika Chuo cha Usafirishaji N.I.T

Katibu Mkuu Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi Mzee Wilson Mukama amewaasa Vijana kupigania maslahi ya Chama na sio kupigania maslahi yao binafsi huku akipinga baadhi ya viongozi ndani ya Chama wanaotambulika kama "Viongozi maslahi".

*"Vijana rushwa ni mbaya sana, epukeni ! Ukithubutu kupewa rushwa huwezi mkosoa kiongozi huyo na hili suala la kukosoana na kujikosoa kwenye Chama chetu ni jambo mtambuka lakini twapaswa kutumia njia sahihi za kukosoana kwenye vikao na kwa kutumia lugha zenye staha"* amesisitiza Mzee Mukama.

Mzee Mukama amewaeleza Vijana na Viongozi wa sasa kurejea kwenye misingi ya Chama cha Mapinduzi kule ilipotoka na amewataka kuwa na desturi ya kusoma vitabu na maandiko mbalimbali yaliyowahi kuadhimiwa na Viongozi waliopita.

Aidha, Katibu Mkuu Mstaafu Ndg.Mukama alisisitiza kwa kusema kuwa Vijana ndio wenye dhamana kubwa ya kuijenga na kuendeleza maendeleo ya Tanzania hivyo wasiogope na wala wasikubali kununuliwa.
Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Mzee Wilson Mukama akipokelewa na Katibu wa Idara ya Organaizesheni, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndg Peter Kasera 
Wanasemina wakimsikiliza Mzee Mukama akihutubia 
"Vijana Amkeni, Nchi inawategemeeni"! Mzee Mukama akisisitiza jambo kwenye semina ya Viongozi
CCM inogireeeee!!!! 

#CCM MPYA

#TANZANIA MPYA

#TUKUTANEKAZINI
Imetolewa na 
Idara yaUhamasishaji na Chipukizi UVCCM TAIFA

No comments